Nokia 8110 4G Mwongozo wa mtumiaji
2. Ili kuchagua ni SIM gani ya kutumia kupiga simu, chagua Simu Zinazotoka , na uchague
SIM1 au SIM2 .
3. Ili kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa ujumbe, chagua Ujumbe Unaotoka , na uchague
SIM1 au SIM2 .
4. Ili kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa data ya simu, chagua Data , na uchague SIM1 au
SIM2 .
Dokezo: Ili kuweza kutofautisha SIM kadi zako, zipe jina la ufafanuzi. Katika mipangilio ya
Kidhibiti SIM , chagua kila SIM kadi, andika jina, na uchague Hifadhi .
Ondoa SIM kadi
Fungua kifuniko cha nyuma, ondoa betri, na uondoe SIM.
Ikiwa una simu ya SIM mbili, telezesha kishikilia SIM2 upande wa kulia na uifungue. Ondoa nano-
SIM, funga kishikiliaji, na uitelezeshe upande wa kushoto ili uifunge mahali pake.
Ondoa kadi ya kumbukumbu
Fungua kifuniko cha nyuma, ondoa betri, na utoe kadi ya kumbukumbu.
Misimbo ya ufikiaji
Simu yako na SIM kadi hutumia misimbo tofauti ya usalama.
• Misimbo ya PIN au PIN2: Misimbo hii hulinda SIM kadi yako dhidi ya matumizi
yasiyoidhinishwa. Ukisahau misimbo au iwe haijatolewa pamoja na kadi yako, wasiliana
na mtoa huduma wa mtandao wako. Ukicharaza msimbo vibaya mara 3 zikifuatana, unahitaji
kufungua msimbo kwa kutumia msimbo wa PUK au PUK2.
• Misimbo ya PUK au PUK2: Misimbo hii inahitajika ili kufungua msimbo wa PIN au PIN2. Ikiwa
misimbo haijatolewa na SIM kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
• Msimbo wa usalama: Msimbo wa usalama hukusaidia kulinda simu yako dhidi ya matumizi
yasiyoidhinishwa. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa usalama ambao
unafasili. Weka msimbo kuwa siri na mahali salama, kando na simu yako. Ukisahau msimbo
na simu yako imefungwa, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada ikatumika,
na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na care
point iliyo karibu ya simu yako, au muuzaji wa simu yako.
• Msimbo wa IMEI: Msimbo wa IMEI hutumiwa kutambua simu katika mtandao. Huenda pia
ukahitaji kupeana nambari kwa huduma zako za care point au muuzaji wa simu. Ili kuona
nambari yako ya IMEI, piga *#06# . Msimbo wa IMEI wa simu yako umechapishwa pia kwenye
lebo ya simu yako, ambayo iko chini ya betri. IMEI inaonekana pia kwenye sanduku halisi la
mauzo.
© 2019 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 10