Nokia 2720 Mwongozo wa mtumiaji
7. Mweko
8. Mikrofoni
9. Kiunganisha vifaa vya kichwa
10. Simu ya SOS/Kisaidizi cha Google/Kitufe
cha utafutaji. Ikiwa umewasha modi
ya ufikiaji, kitufe hutuma simu ya SOS.
Vinginevyo, kitufe huwasha Kisaidizi cha
Google. Kisaidizi cha Google hupatikana
katika masoko na lugha zilizoteuliwa.
Ambapo hakipatikani, Kisaidizi cha Google
hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google.
11. Kipenyo cha kufungua kifuniko cha nyuma
12. Kiunganisha USB
13. Kipaza sauti
14. Vitufe vya sauti
15. Kitufe cha uchaguzi cha kulia
16. Kitufe cha nyuma
17. Kitufe cha nishati/kukata simu
18. Mikrofoni
Ili kufungua vitufe, fungua mkunjo.
Jiepushe kugusa eneo la antena bila sababu wakati antena inatumika. Ugusaji antena huathiri
ubora wa mawasiliano na unaweza kupunguza maisha ya betri kwa sababu ya kiwango cha juu
zaidi cha nishati wakati wa utendaji kazi.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au kifaa chochote cha kichwa kando na zile zilizoidhinishwa kutumiwa
na kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti. Sehemu nyingine
za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke kadi za karadha
au vitu vingine vyenye kutumia hifadhi ya sumaku karibu na kifaa hiki, kwa sababu maelezo
yaliyohifadhiwa kwenye vitu hivyo yanaweza kufutika.
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika kiongozi hiki, kama vile chaja, kifaa cha kichwani, au
kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
SANIDI NA UWASHE SIMU YAKO
Jifunze jinsi ya kuingiza SIM kadi, kadi ya kumbukumbu, na betri, na jinsi ya kuwasha simu yako.
Nano-SIM
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi ya nano pekee tu (angalia mfano).
Matumizi ya kadi zisizotangamana za SIM zinaweza kuharibu kadi au kifaa, na zinaweza
kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
© 2019 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 7