Nokia 215 4G instrukcja

Typ
instrukcja
Mwongozo wa mtumiaji
Toleo 2020-12-18 sw
Mwongozo wa mtumiaji
1 Kuhusu mwongozo huu wa mtumiaji
Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 2
Mwongozo wa mtumiaji
Yaliyomo
1 Kuhusu mwongozo huu wa mtumiaji 2
2 Yaliyomo 3
3 Anza kutumia 5
Vitufe na sehemu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5
Sanidi na uwashe simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6
Chaji simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9
Vitufe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9
4 Simu, majina, na ujumbe 11
Simu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11
Majina . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11
Tuma ujumbe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12
5 Binafsisha simu yako 13
Badilisha toni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13
Badilisha mwonekano wa skrini yako ya mwanzo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13
Pata mengi kutoka kwa SIM kadi mbili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13
6 Intaneti na miunganisho 14
Vinjari wavuti . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14
Bluetooth® . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14
7 Muziki 15
Kicheza muziki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
Sikiliza redio . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
8 Saa, kalenda, na kikokotoo 16
Weka saa na tarehe wewe mwenyewe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
Saa ya kengele . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
Kalenda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
Kikokotoo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 3
Mwongozo wa mtumiaji
9 Safisha simu yako 18
Ondoa maudhui binafsi kwenye simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 18
10 Maelezo ya bidhaa na usalama 19
Kwa usalama wako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19
Simu za dharura . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21
Kuhudumia kifaa chako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22
Uchakataji upya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
Alama ya pipa iliyo na mkato . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
Maelezo ya betri na chaja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
Watoto wadogo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
Vifaa vya matibabu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
Vifaa vya kusaidia kusikia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Linda kifaa chako dhidi ya maudhui mabaya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Magari . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Mazingira yanayoweza kulipuka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Habari ya utoaji cheti (SAR) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26
Kuhusu Usimamizi wa haki za Dijitali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 27
Hakimiliki na ilani nyingine . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 27
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 4
Mwongozo wa mtumiaji
3 Anza kutumia
VITUFE NA SEHEMU
Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji unatumika kwa modeli zifuatazo: TA-1272, TA-1264, TA-1284, TA-
1281, TA-1278, TA-1280.
1. Kitufe cha kutembeza
2. Maikrofoni
3. Kitufe cha kupiga simu
4. Kitufe cha uchaguzi cha kushoto
5. Kifaa cha masikio
6. Kiunganisha vifaa vya kichwa
7. Tochi
8. Kitufe cha uchaguzi cha kulia
9. Kitufe cha nishati/kukata simu
10. Kipaza sauti
11. Kipenyo cha kufungua kifuniko cha nyuma
12. Kiunganisha USB
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 5
Mwongozo wa mtumiaji
Jiepushe kugusa eneo la antena bila sababu wakati antena inatumika. Unganisha na antena
huathiri ubora wa mawasiliano na unaweza kupunguza maisha ya betri kwa sababu ya kiwango
cha juu zaidi cha nishati wakati wa uendeshaji.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au kifaa chochote cha kichwa kando na zile zilizoidhinishwa kutumiwa
na kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti. Sehemu nyingine
za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke kadi za karadha
au vitu vingine vyenye kutumia hifadhi ya sumaku karibu na kifaa hiki, kwa sababu maelezo
yaliyohifadhiwa kwenye vitu hivyo yanaweza kufutika.
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwani, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
Dokezo: Unweza kuweka simu yako kuulizia msimbo wa usalama ili kulinda faragha na data
yako ya kibinafsi. Chagua Menyu > > Usalama > Kilinda vitufe > Msimbo wa usalama .
Hata hivyo kumbuka, kwamba unahitaji kukumbuka msimbo, kwa kuwa HMD Global haiwezi
kuufungua au kuuruka.
SANIDI NA UWASHE SIMU YAKO
Nano-SIM
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi ya nano pekee (angalia mfano).
Matumizi ya kadi zisizotangamana za SIM zinaweza kuharibu kadi au kifaa, na zinaweza
kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kumbuka: Zima kifaa na usiiunganishe na chaja au kifaa kingine chochote kabla ya kubandua
vifuniko vyovyote. Epuka kugusa visehemu vya elektroniki wakati wa kubadilisha vifuniko
vyovyote. Daima hifadhi na kutumia kifaa kikiwa na vifuniko vyake vimewekwa.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 6
Mwongozo wa mtumiaji
Fungua kifuniko cha nyuma
1. Weka kucha yako ya kidole katika nafasi ndogo chini ya simu, inua na uondoe kifuniko.
2. Ikiwa betri iko ndani ya simu, itoe.
Ingiza SIM kadi
1. Telezesha kishikio cha SIM kadi upande wa kushoto na ukifungue.
2. Weka nano-SIM katika nafasi ya SIM ikiangalia chini.
3. Funga kishikiliaji, na uitelezeshe upande wa kulia ili uifunge mahali pake.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 7
Mwongozo wa mtumiaji
Ingiza SIM ya pili
1. Telezesha kishikilia SIM kadi cha kipenyo cha SIM2 upande wa kulia na uifungue.
2. Weka nano-SIM katika kipenyo cha SIM2 ikiangalia chini.
3. Funga kishikiliaji, na ukitelezeshe upande wa kushoto ili ukifunge mahali pake. SIM kadi
zote zinapatikana kwa wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini ijapokuwa SIM kadi moja
inatumika, kwa mfano, kwa kupiga simu, ile nyingine haipatikani.
Kidokezo: Ili kujua ikiwa simu yako inaweza kutumia SIM kadi 2, angalia lebo kwenye sanduku
la mauzo. Ikiwa kuna misimbo 2 ya IMEI kwenye lebo, una simu yenye SIM mbili.
Ingiza kadi ya kumbukumbu
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 8
Mwongozo wa mtumiaji
1. Telezesha kadi ya kumbukumbu kwenye nafasi ya kadi ya kumbukumbu.
2. Rudisha betri.
3. Rejesha kifuniko cha nyuma.
Washa simu yako
Bonyeza na ushikilie .
CHAJI SIMU YAKO
Betri yako imechajiwa nusu kiwandani, lakini utahitajika kuichaji upya kabla uweze kutumia simu
yako.
Chaji betri
1. Chomeka chaja kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha chaja kwenye simu. Ukimaliza, chomoa chaja kwenye simu, kisha kwenye soketi
ya ukuta.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
Kidokezo: Unaweza kuchaji kwa kutumia USB wakati umeme wa ukutani haupatikani. Data
inaweza kuhamishwa ukichaji kifaa. Ubora wa nishati ya kuchaji kwa USB hutofautiana,
na huenda ikachukua muda mrefu kuchaji kuanza na kifaa kuanza kufanya kazi. Hakikisha
kompyuta yako imewashwa.
VITUFE
Tumia vitufe vya simu
Ili kuona programu na vipengele vya simu yako, kwenye skrini ya mwanzo, chagua Menyu .
Ili kwenda kwenye programu au kipengele, bonyeza kitufe cha kutambaza juu, chini,
kushoto, au kulia. Ili kufungua programu au kipengele, bonyeza kitufe cha kutambaza.
Funga vitufe
Ili kuepuka kubonyeza vitufe kwa bahati mbaya, funga vitufe. bonyeza . Ili ufungue vitufe,
bonyeza kitufe cha kutembeza, na uchague Fungua > * .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 9
Mwongozo wa mtumiaji
Andika kwa kutumia kitufe
Bonyeza kitufe kisha utumie kitufe cha kutembeza ili uchague herufi unayotaka.
Ili kucharaza katika nafasi bonyeza 0 .
Ili kucharaza kibambo maalum au alama ya kituo, chagua > Ingiza chaguo > Ingiza alama .
Ili kubadilisha kati ya vibambo, bonyeza # kwa kurudia.
Ili kuandika nambari, bonyeza kitufe cha nambari na utumie kitufe cha kutembeza ili uchague
nambari.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 10
Mwongozo wa mtumiaji
4 Simu, majina, na ujumbe
SIMU
Piga simu
Jifunze jinsi ya kupiga simu kwa kutumia simu yako mpya.
1. Ingiza namba ya simu. Ili kucharaza kibambo cha +, kinachotumiwa kwa simu za kimataifa,
bonyeza * mara mbili.
2. Bonyeza . Ukiulizwa, chagua ni SIM gani ya kutumia.
3. Kukata simu, bonyeza .
Jibu simu
Bonyeza .
MAJINA
Ongeza jina
1. Chagua Menyu > > + Mwasiliani mpya .
2. Andika jina, na ucharaze nambari.
3. Chagua > Sawa .
Ili kuongeza waasiliani zaidi, chagua > Ongeza mwasiliani mpya .
Hifadhi mwasiliani kutoka kwenye rekodi ya simu
1. Chagua Menyu > .
2. Tembeza kwa nambari unataka kuhifadhi, chagua > Ongeza kwa Waasiliani >
Mwasiliani mpya .
3. Ongeza jina la mwasiliani, kagua kwamba nambari ya simu ni sahihi, na uchague > Sawa .
Pigia simu mwasiliani
Unaweza kupigia simu mwasiliani moja kwa moja kutoka kwenye orodha ya waasiliani.
Chagua Menyu > , tembeza kwa mwasiliani unataka kupigia simu, na ubonyeze kitufe cha
kupiga simu.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 11
Mwongozo wa mtumiaji
TUMA UJUMBE
Andika na utume ujumbe
1. Chagua Menyu > > + Ujumbe mpya .
2. Katika sehemu ya Wapokeaji, ingiza
nambari ya mpokeaji, au uchague >
Waasiliani ili kuongeza waasiliani kutoka
kwa orodha yako ya waasiliani.
3. Andika ujumbe kwenye sehemu ya ujumbe.
4. Ili kuingiza smaili au alama kwenye ujumbe,
chagua > Chaguo za kuingiza >
Ingiza smaili au Ingiza alama .
5. Chagua Tuma .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 12
Mwongozo wa mtumiaji
5 Binafsisha simu yako
BADILISHA TONI
Weka toni mpya
1. Chagua Menyu > > Ubinafsishaji > Sauti .
2. Chagua toni unataka kubadilisha.
3. Telezesha kwenye toni unataka na uchague Chagua .
BADILISHA MWONEKANO WA SKRINI YAKO YA MWANZO
Chagua pazia mpya
Unaweza kubadilisha madharinyuma ya skrini yako ya mwanzo.
1. Chagua Menyu > > Ubinafsishaji > Funga mandharinyuma ya skrini > Pazia .
2. Telezesha mandharinyuma unataka na uchague Chagua .
3. Ikiwa umependezwa na pazia, chagua .
PATA MENGI KUTOKA KWA SIM KADI MBILI
Simu yako inaweza kuwa na SIM kadi mbili, na unaweza kuzitumia kwa malengo tofauti.
Chagua ni SIM kadi gani itatumika
Chagua Menyu > > Muunganisho > SIM Mbili .
Ili kuchagua SIM gani ya kutumia kupiga simu, chagua SIM inayopendelewa kupiga simu .
Kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa ujumbe, chagua SIM inayopendelewa ya ujumbe .
Kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa data ya simu, chagua Muunganisho wa data ya simu >
SIM unayopendelea .
Dokezo: Unaweza kuweka jina jipya la SIM kadi zako ili iwe rahisi kuzitofautisha. Chagua
Menyu > > Muunganisho > SIM mbili > Mipangilio ya SIM . Chagua SIM na jina la SIM .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 13
Mwongozo wa mtumiaji
6 Intaneti na miunganisho
VINJARI WAVUTI
Unganisha kwenye intaneti
Kumbuka kwamba huenda kivinjari kikatofautiana na eneo lako na kufanya kazi kitofauti.
1. Chagua Menyu > .
2. Andika anwani ya wavuti, na ubonyeze Sawa .
BLUETOOTH®
Unganisha simu yako kwenye vifaa vingine kwa kutumia Bluetooth.
Washa Bluetooth
1. Chagua Menyu > > Muunganisho > Bluetooth .
2. Washa Bluetooth .
3. Chagua Vifaa vinavyopatikana na kifaa cha Bluetooth unataka kuunganisha.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 14
Mwongozo wa mtumiaji
7 Muziki
KICHEZA MUZIKI
Unaweza kusikiliza faili zako za muziki wa MP3 kwa kutumia kicheza muziki.
Sikiliza muziki
Kucheza muziki, unahitaji kuhifadhi faili za muziki kwenye kadi ya kumbukumbu au
kumbukumbu ya simu.
1. Chagua Menyu > .
2. Chagua Nyimbo ili uone muziki wako wote uliohifadhiwa.
3. Tembeza kwa wimbo na uchague Cheza .
Unaweza pia kuunda orodha yako mwenyewe ya kucheza.
Ili kurekebisha sauti, tembeza juu au chini.
SIKILIZA REDIO
Sikiliza kituo chako ukipendacho cha redio kwenye simu yako
Chagua Menyu > . Simu yako hutafuta vituo kiotomatiki unapowasha redio. Ili kubadilisha
sauti, tembeza juu au chini. Ili kuhifadhi kituo, chagua > Ongeza kwenye vipendwa . Ili
kubadilisha kwa kituo kilichohifadhiwa, chagua > Vipendwa , na uchague kituo. Ili kufunga
redio, chagua > Funga redio .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 15
Mwongozo wa mtumiaji
8 Saa, kalenda, na kikokotoo
WEKA SAA NA TAREHE WEWE MWENYEWE
Badilisha saa na tarehe
1. Chagua Menyu > > Saa na tarehe >
Tarehe na saa .
2. Zima Sasisha kiotomatiki .
3. Ili kuweka saa, chagua Saa na uingize saa.
4. Ili kuweka tarehe, chagua Tarehe na
uingize tarehe.
5. Chagua Hifadhi .
SAA YA KENGELE
Jifunze jinsi ya kutumia saa ya kengele ili kukuamsha na ufike maeneo kwa wakati unaofaa.
Weka kengele
Huna saa? Tumia simu yako kama saa ya kengele.
1. Chagua Menyu > .
2. Chagua + Kengele mpya na uingize saa ya kengele na maelezo mengine.
3. Chagua > Hifadhi .
KALENDA
Ungependa kukumbuka tukio? Iongeze kwenye kalenda yako.
Ongeza tukio la kalenda
1. Chagua Menyu > .
2. Chagua tarehe na + Tukio lipya .
3. Ingiza maelezo ya tukio, na uchague Hifadhi .
KIKOKOTOO
Jifunze jinsi ya kuongeza, kuondoa, kuzidisha na kugawanya kwa kutumia kikokotoo cha simu
yako.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 16
Mwongozo wa mtumiaji
Jinsi ya kuhesabu
1. Chagua Menyu > .
2. Ingiza nambari ya kwanza ya hesabu yako, tumia kitufe cha kutembeza ili uchague shughuli,
na uingize nambari ya pili.
3. Bonyeza kitufe cha kutambaza ili upate matokeo ya hesabu hiyo.
Chagua ili kufuta sehemu za nambari.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 17
Mwongozo wa mtumiaji
9 Safisha simu yako
ONDOA MAUDHUI BINAFSI KWENYE SIMU YAKO
Ukinunua simu mpya, au uwe unataka kutupa au kuchakata upya simu yako, hivi ndivyo
unavyoweza kuondoa maelezo na maudhui yako ya kibinafsi. Kumbuka kwamba ni wajibu wako
kuondoa maudhui yote ya kibinafsi.
Ondoa maudhui kwenye simu yako
Wakati unaondoa maudhui ya kibinafsi kwenye simu yako, zingatia kama unaondoa maudhui
kwenye kumbukumbu ya simu au SIM kadi.
Ili kuondoa ujumbe, chagua Menyu > . Chagua > Futa mazungumzo , chagua ujumbe zote
na .
Ili kuondoa waasiliani, chagua Menyu > . Chagua > Futa waasiliani , chagua waasiliani
wote na .
Ili kuondoa maelezo yako ya simu, chagua Menyu > . Chagua > Futa zote > Sawa .
Kagua ikiwa maudhui yote ya kibinafsi yameondolewa.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 18
Mwongozo wa mtumiaji
10 Maelezo ya bidhaa na usalama
KWA USALAMA WAKO
Soma maelekezo haya rahisi. Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au kinyume cha sheria na
masharti. Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo kamili wa mtumiaji.
ZIMA KATIKA MAENEO YALIYOKATAZWA
Zima kifaa wakati matumizi ya simu za mkononi yamekatazwa au wakati yanaweza kusababisha
mwingiliano au hatari, kwa mfano, ndani ya ndege au hospitalini, au karibu na vifaa vya
matibabu, mafuta, kemikali, au maeneo yenye mlipuko. Tii maagizo yote katika maeneo
yaliyozuiwa.
USALAMA BARABARANI HUJA KWANZA
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima iache mikono yako iwe huru wakati unaendesha gari. Kitu
cha kuzingatia kwanza unapoendesha gari unapaswa kuwa usalama barabarani.
MWINGILIANO
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 19
Mwongozo wa mtumiaji
Vifaa vyote visivyotumia waya vina uwezekano wa kupata mwingiliano, ambao unaweza kuathiri
utendaji kazi wake.
HUDUMA ILIYOIDHINISHWA
Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kuweka au kukarabati bidhaa hii.
BETRI, CHAJA, NA VIFAA VINGINE VYA ZIADA
Tumia betri, chaja, na vifaa vya ziada ambavyo vimeidhinishwa na HMD Global Oy kwa ajili ya
matumizi na kifaa hiki tu. Usiunganishe bidhaa ambazo haziendani pamoja.
WEKA KIFAA KIKIWA KIKAVU
Ikiwa kifaa chako kinaweza kuzuia maji, tafadhali rejelea ukadiriaji wake wa IP kwa mwongozo
zaidi wa kina.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 20
  • Page 1 1
  • Page 2 2
  • Page 3 3
  • Page 4 4
  • Page 5 5
  • Page 6 6
  • Page 7 7
  • Page 8 8
  • Page 9 9
  • Page 10 10
  • Page 11 11
  • Page 12 12
  • Page 13 13
  • Page 14 14
  • Page 15 15
  • Page 16 16
  • Page 17 17
  • Page 18 18
  • Page 19 19
  • Page 20 20
  • Page 21 21
  • Page 22 22
  • Page 23 23
  • Page 24 24
  • Page 25 25
  • Page 26 26
  • Page 27 27
  • Page 28 28

Nokia 215 4G instrukcja

Typ
instrukcja