Nokia 5310 Mwongozo wa mtumiaji
Chaji betri
1. Chomeka chaja kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha chaja kwenye simu. Ukimaliza, chomoa chaja kwenye simu, kisha kwenye soketi
ya ukuta.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
Kidokezo: Unaweza kuchaji kwa kutumia USB wakati umeme wa ukutani haupatikani. Data
inaweza kuhamishwa ukichaji kifaa. Ubora wa nishati ya kuchaji kwa USB hutofautiana,
na huenda ikachukua muda mrefu kuchaji kuanza na kifaa kuanza kufanya kazi. Hakikisha
kompyuta yako imewashwa.
VITUFE
Tumia vitufe vya simu
• Ili kuona programu na vipengele vya simu
yako, kwenye skrini ya mwanzo, chagua
Menyu .
• Ili kwenda kwenye programu au kipengele,
bonyeza kitufe cha kutambaza juu,
chini, kushoto, au kulia. Ili kufungua
programu au kipengele, bonyeza kitufe
cha kutambaza.
• Kurudi kwa skrini ya mwanzo, bonyeza
kitufe cha kukata simu .
• Kubadilisha sauti ya simu yako, bonyeza
kitufe cha kuongeza na kupunguza sauti.
• Ili kuwasha tochi, kwenye skrini ya
mwanzo, bonyeza kitufe cha kutekezesha
juu mara mbili. Ili kuzima, telezesha juu
mara moja. Usimulike taa katika macho ya
mtu yeyote.
Funga vitufe
Ili kuepuka kubonyeza vitufe kwa bahati mbaya, funga vitufe. chagua Nenda kwa >
Funga vitufe . Ili kufua kitufe, bonyeza , na uchague Fungua .
ANDIKA MATINI
Andika kwa kutumia kibeba matini
Bonyeza kitufe kwa kurudia hadi herufi ionyeshwe.
Ili kucharaza katika nafasi, bonyeza kitufe cha 0.
Kucharaza kibambo maalum au alama ya kituo, bonyeza kitufe cha asteriki *, au ikiwa unatumia
kamusi, bonyeza na ushikilie kitufe cha asteriki.
Ili kubadilisha kati ya vibambo, bonyeza kitufe cha # kwa kurudia.
Ili kucharaza nambari, bonyeza na ushikilie kitufe cha nambari.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 9