Mwongozo wa mtumiaji
Jiepushe kugusa eneo la antena bila sababu wakati antena inatumika. Unganisha na antena
huathiri ubora wa mawasiliano na unaweza kupunguza maisha ya betri kwa sababu ya kiwango
cha juu zaidi cha nishati wakati wa uendeshaji.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au kifaa chochote cha kichwa kando na zile zilizoidhinishwa kutumiwa
na kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti. Sehemu nyingine
za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke kadi za karadha
au vitu vingine vyenye kutumia hifadhi ya sumaku karibu na kifaa hiki, kwa sababu maelezo
yaliyohifadhiwa kwenye vitu hivyo yanaweza kufutika.
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwani, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
Dokezo: Unweza kuweka simu yako kuulizia msimbo wa usalama ili kulinda faragha na data
yako ya kibinafsi. Chagua Menyu > > Usalama > Kilinda vitufe > Msimbo wa usalama .
Hata hivyo kumbuka, kwamba unahitaji kukumbuka msimbo, kwa kuwa HMD Global haiwezi
kuufungua au kuuruka.
SANIDI NA UWASHE SIMU YAKO
Nano-SIM
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi ya nano pekee (angalia mfano).
Matumizi ya kadi zisizotangamana za SIM zinaweza kuharibu kadi au kifaa, na zinaweza
kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kumbuka: Zima kifaa na usiiunganishe na chaja au kifaa kingine chochote kabla ya kubandua
vifuniko vyovyote. Epuka kugusa visehemu vya elektroniki wakati wa kubadilisha vifuniko
vyovyote. Daima hifadhi na kutumia kifaa kikiwa na vifuniko vyake vimewekwa.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 6